Saratani ya matiti (breast cancer)
Maana Rahisi
Saratani ya matiti ni aina ya saratani inayojitokeza kwenye tishu za matiti. Inaweza kuathiri wanawake na wanaume, ingawa inajitokeza zaidi kwa wanawake.
Vihatarishi
Vihatarishi:
• Umri: Hatari ya kupata saratani ya matiti huongezeka kwa umri, hasa baada ya miaka 50.
• Historia ya familia: Kuwa na historia ya saratani ya matiti katika familia.
• Jeni: Mabadiliko ya jeni za BRCA1 na BRCA2 yanaongeza hatari.
• Homoni za uzazi: Utoaji wa homoni za uzazi kwa muda mrefu, hasa baada ya kumaliza hedhi.
• Kuanza hedhi mapema: Kuanza hedhi kabla ya miaka 12.
• Kuzaa kwa umri mkubwa: Kuzaa mtoto wa kwanza baada ya miaka 30 au kutokuzaa kabisa.
• Kutokunyonyesha: Kutokunyonyesha watoto kunaweza kuongeza hatari.
• Lishe yenye mafuta mengi: Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na nyuzi nyuzi chache.
• Unene kupita kiasi: Kuwa na uzito kupita kiasi au unene kupita kiasi.
• Kuvuta sigara na unywaji pombe: Kuvuta sigara na kunywa pombe kwa wingi.
Dalili na Ishara.
- • Uvimbe kwenye titi: Kuwapo kwa uvimbe usio wa kawaida kwenye titi au kwapani. • Mabadiliko ya ukubwa au umbo la titi: Titi moja kuwa kubwa au kubadilika umbo. • Kubadilika kwa ngozi ya titi: Ngozi ya titi kuwa na mabadiliko kama ngozi ya chungwa (dimpling). • Mabadiliko ya chuchu: Chuchu kuvutwa ndani au kutoa uchafu wa damu. • Maumivu kwenye titi: Maumivu yasiyo ya kawaida kwenye titi au kwapani. • Kubadilika kwa rangi ya ngozi: Ngozi ya titi kuwa na rangi isiyo ya kawaida, nyekundu au nyeusi.
Uchunguzi.
• Mammogram: Picha za X-ray za matiti ili kuona uvimbe au mabadiliko kwenye tishu za matiti.
• Ultrasound: Kipimo cha ultrasound cha matiti ili kuona uvimbe na kugundua kama ni mfupa au majimaji.
• Biopsy: Kuchukua sampuli ya tishu kutoka kwenye uvimbe ili kuchunguza seli za saratani.
• MRI: Picha za mwili ili kuona ukubwa wa saratani na kama imeenea sehemu nyingine za mwili.
• CT scan na PET scan: Picha za mwili ili kuona kama saratani imeenea sehemu nyingine za mwili.
Matibabu
• Upasuaji: Kuondoa uvimbe au titi lote kulingana na hatua ya saratani.
o Lumpectomy: Kuondoa uvimbe pekee na tishu chache zinazozunguka.
o Mastectomy: Kuondoa titi lote.
• Radiotherapy: Matumizi ya mionzi kuua seli za saratani baada ya upasuaji.
• Chemotherapy: Matumizi ya dawa za kuua seli za saratani kabla au baada ya upasuaji.
• Hormone therapy: Matumizi ya dawa za kupunguza au kuzuia homoni za uzazi zinazochochea ukuaji wa saratani.
• Targeted therapy: Matumizi ya dawa zinazolenga protini maalum kwenye seli za saratani.
• Immunotherapy: Matumizi ya dawa zinazosaidia mfumo wa kinga kupambana na saratani.
Kinga.
• Vipimo vya mara kwa mara: Kufanya vipimo vya mammogram mara kwa mara kwa wanawake wote walioko kwenye umri wa hatari.
• Kujichunguza matiti: Kujichunguza matiti mwenyewe mara kwa mara ili kugundua mabadiliko yoyote.
• Lishe bora: Kula lishe yenye mboga, matunda, na nyuzi nyuzi nyingi.
• Mazoezi ya mara kwa mara: Kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kudumisha uzito bora na afya njema.
• Kuepuka pombe na sigara: Kuacha kunywa pombe kwa wingi na kuvuta sigara.
• Kunyonyesha watoto: Kunyonyesha watoto kunaweza kupunguza hatari ya saratani ya matiti.
• Kujua historia ya familia: Kujua historia ya familia na kuchukua hatua mapema kama kuna hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti.
• Matumizi ya tiba ya homoni kwa uangalifu: Kuepuka matumizi ya muda mrefu ya tiba ya homoni baada ya kumaliza hedhi.
Experience convenience, reliability, and personalized care with Tube Medical Services! Contact us today for a healthier tomorrow!
#TubeMedical #HealthMatters #WellnessJourney #tanzania #daressalaam #afya #drmbashu #drissambashu #HealthcareRevolution #OnlineConsultation