Saratani ya Shingo ya Kizazi (Cervical Cancer)
Saratani ya shingo ya kizazi ni aina ya saratani inayojitokeza kwenye seli za shingo ya kizazi, sehemu ya chini ya mfuko wa uzazi unaounganisha na uke. Saratani hii husababishwa na mabadiliko yasiyo ya kawaida ya seli kutokana na maambukizi ya virusi vya Human Papillomavirus (HPV).